Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mgaywa atamba kuipeleka ADC Ikulu Uchaguzi Mkuu 2025

Muktasari:

  • Mgaywa kabla ya kupewa mkoba wa kuipeperusha bendera ya ADC kwenye Uchaguzi Mkuu Oktoba, mwaka huu, amewahi kuwa mbunge wa Mwibara mkoani Mara (1995-2005) kwa tiketi ya TLP.

Dar es Salaam. Chama cha Alliance for Democratic Change (ADC), kimemtangaza mwanasiasa mkongwe, Mutamwega Mgaywa kuwa mgombea urais katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu kwa tiketi ya chama hicho.

Mgaywa ambaye amewahi kuwa mbunge wa Mwibara mkoani Mara (1995-2005), kwa tiketi ya TLP amejiunga na ADC kisha kukabidhiwa bendera ya chama hicho kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu.

Uamuzi wa kumtangaza Mgaywa kugombea nafasi hiyo umetangazwa leo Mei 23, 2025, na Katibu Mkuu wa ADC taifa, Hamad Aziz jijini Dar es Salaam.

“Kazi iliyotuleta mbele yenu ni mtia nia amekuja kuchukua fomu ya kugombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia ADC,” amesema Aziz.

Akizungumza baada ya kumkabidhi fomu hiyo, Makamu Mwenyekiti wa ADC bara, Hassan Mvungi amesema Mgaywa sasa atasubiria kukamilisha mchakato wa ndani ya chama ikiwemo kupitishwa na Mkutano Mkuu maalum wa chama cha ADC.

“Chama cha ADC kitaendelea kusimama imara katika kuhakikisha Demokrasia, haki na maendeleo vinapewa kipaumbele. Tunakutakia kila la heri katika hatua zilizobakia kwenye mchakato wa ndani ya chama,” amesema Mvungi.


Alichosema Mugaywa

Akizungumza baada ya kukabidhiwa mkoba wenye fomu ya kugombea urais, Mutamwega Mugaywa amesema siku zote amekuwa na kiu ya kuwatumikia Watanzania katika wadhfa huo huku akijigamba kuwa anaamini ndoto hiyo itatimia mwaka huu.

“Safari hızı tunaamini kwamba ikimpendeza Mungu tutakuwa ndani ya Ikulu na kumbukeni baba wa taifa (Julius Nyerere) aliwahi kusema watu wakuhitaji ndiyo wewe uchukue fomu,” amesema Mgaywa.

Mgaywa amesema kabla ya kuchukua uamuzi wa kutangaza nia kugombea urais kupitia ADC, alifuatwa na vyama sita vya siasa (bila kuvitaja) vikimtaka apeperushwe bendera zao kwenye nafasi ya urais kwenye uchaguzi ujao.

“ADC ni chama tulivu, kinajali muungano, kinapenda amani na pia kina malengo ya maendeleo. Nimeanza safari yangu kutokea kijijini hadi Dar es Salaam na nimekabidhiwa fomu rasmi ya kuwa mgombea urais,” amesema.

Amesema anatambua umma unamjua kwa msimamo wake, mpenda haki na maendeleo, hivyo ataipeerusha bendera ya ADC kufikia lengo la kuongoza nchi na kukiwezesha chama hicho kuingia Ikulu ya Tanzania.

“Wanachama wetu wamesema mimi nahitajika kwa hali hiyo nina uhakika kwamba wameona uwezo wangu, watanipa urais wa nchi hii halafu tufanye mambo ya maendeleo,” amesema.


OSZAR »