Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Rais Samia ataka ‘magwajima’ waachwe nje CCM

Muktasari:

  • Rais Samia amebainisha hayo leo Mei 30, 2025 jijini Dodoma wakati akihitimisha mkutano mkuu maalumu wa CCM uliofan-yika kwa siku mbili ambapo ajenda mba-limbali zimejadiliwa ikiwemo taarifa ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya mwaka 2020 na uzinduzi wa ilani mpya ya 2025/30.

Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Rais Samia Suluhu Has-san amewataka wajumbe wa vikao vya uchujaji kwenda kufanya uchujaji wa haki na uadilifu wakati wa mchakato wa kupata wagombea huku akiagiza wale “magwaji-ma” waachwe nje.

Rais Samia amebainisha hayo leo Mei 30, 2025 jijini Dodoma wakati akihitimisha mkutano mkuu maalumu wa CCM uliofanyika kwa siku mbili ambapo ajenda mba-limbali zimejadiliwa ikiwemo taarifa ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya mwaka 2020 na uzinduzi wa ilani mpya ya 2025/30.

Rais Samia amesisitiza kuachwa 'magwajima' katika mchujo wa wagombea huku akisisitiza haki na weledi katika mchakato huo. “Tukitoa mwanya ndugu zangu, tukipitisha wale wanaotaka na mie niwemo, ndiyo tunapata wale wanaokwenda huko, chama kinakuwa Gwajimanized. Kwa vyovyote vile, tusigwajimanize chama chetu, magwajima tuyaache nje, hamna kuoneana aibu wala haya."

Jana, siku ya kwanza ya mkutano huo, Rais Samia alisema kama kuna mwanaCCM anayewaza kukpasua chama hicho ajitafa-kari. Alisema chama hicho kuwa maendeleo makubwa, maana yake kinakua, kina wap-enzi na mashabiki wengi.

Alisisitiza kuwa pindi jengo la makao makuu ya CCM litakapokamilika ujenzi wake, litakuwa ni ishara ya ukuaji na uimara wa chama, akiwataka wanachama wote ku-shirikiana katika kukitumikia kwa umoja badala ya kukipasua.

Akizungumza wakati wa hotuba yake, leo, Rais Samia amesema kwa kuangalia tu hali ilivyo, CCM tayari imeshinda, kwa wingi wa wananchama, kwani wakitoka wanachama wao wote kupiga kura, na wapenzi wao wakapiga kura, wanakuwa na kura nyingi.

Amesisitiza kwamba ni jukumu lao wote kwenda kunadi ilani na kuwataka wanachama na wapenzi wao kujitokeza kupiga kura. Amewaomba kuwa umoja, up-endo na mshikamano katika kipindi hiki cha uchaguzi.

Mwenyekiti huyo wa CCM ameagiza vikao vinavyokwenda kuchuja wagombea, wakatende haki. Amesema anayefaa aambiwe anafaa, asiyefaa, aambiwe ana kasoro moja mbili tatu, lakini hafai kwa huko mbele wanakokwenda.

Amesema kule Zanzibar, kuna usemi usemao “mcheza ngoma si yake, lazima ataharibu”, kwa maana ya kwamba hawi sawa na wenzake, yeye anakuwa ma-judhubu, akieleza kwamba majudhubu maana yake ni “mtu ambaye hazimo.”

“Ukicheza ngoma si yako lazima utaharibu na utajulikana tu, lazima utasema mie siye jamani, ndiyo haya yanayotokea. Kwa hiyo twendeni tukachuje kwa ustadi mkubwa, tukaweke watu ambao watakifanyia kazi chama chetu, tutakwenda kutekeleza,” amesema Rais Samia.

Ameongeza kuwa: “Ili tuwe na uchujaji wenye haki na uadilifu, wale walio kwenye vikao vya uchujaji ambao wana nia ya ku-gombea, tunaomba watoe taarifa mapema, watupishe. Upande wa serikali tulishapata majina, bado upande wa chama.”

“Tukikuacha mpaka uchukue fomu, tayari utakuwa umesababisha hasara kwa wenzio. Nimemwambia katibu mkuu, ifikapo Juni Mosi, tayari tuwe tumepata majina ya wenye nia ya kugombea, lengo ni kwamba tunataka kuziingiza kwenye mafunzo ka-mati za siasa na kamati zote zitakazokaa kwenye uchujaji.”


Wanaosema wametumwa

Rais Samia ametahadharisha kuhusu wanaokwenda kwenye majimbo na kusema wametumwa kugombewa na wengine wakisemewa kwamba wametumwa, ame-wahakikishia kwamba yeye na Rais wa Zanzibar hawajamtuma mtu kwenda kugombea.

“Hatutatuma watu kuja majimboni, sisi tu-na nafasi zetu 10, kwa hiyo tukimaliza uchaguzi kwa watu tunaowataka, tuna nafasi zetu 10. Kwa hiyo, mlioko kwenye majimbo mjizatiti na majimbo yenu na msi-fanye uoga, mkiona watu mnasema wame-tumwa.

“Hao wanaojileta wakasema wametumwa, wakateni mapema sana. Hatujatuma watu, huu ni uwanja wa wazi, kila mtu ajipime uwezo wake aingie kwenye mchezo, hazuiwi mtu, wananchi kule wataamua nani wanamtaka, lakini tukimaliza kuamua, chama kirudi kuwa kimoja,” amesema.

Ameongeza kuwa: “Nawaomba sana, mnapoenda kuchuja, tuleteeni watakaowe-za kazi ya kumarisha ustawi wa watu na taifa letu kwa ujumla, siyo tu mtu kaja ili mradi kaja, mtu ambaye tukimpa kazi ata-beba na atafanya, mtu ambaye anajua nimechukua jimbo na wajibu wangu ni nini kwenye jimbo.”

Mwenyekiti huyo wa CCM Taifa, amevitaka vikao vya uchujaji kwenda kutenda haki na uadilifu wakati wa mchakato wa kuwatafu-ta wagombea huku akisisitiza kwamba ni jukumu la kila mwanachama kuinadi ilani ya chama hicho kwenye uchaguzi ujao.


Maoni ya wadau

Mchambuzi wa siasa, Ramadhan Manyeko amesema anapingana kidogo na Mwenyeki-ti wa CCM, Rais Samia, akisema mara nyingi wagombea wazuri wanaachwa kwenye mchakato wa kura za maoni badala yake wanachukuliwa wenye uwezo wa kifedha.

“Kwa nyakati tofauti tumekuwa tukishuhudia malalamiko kuhusu mchakato wa kura za maoni za kuwapata wagombea wa udiwani na ubunge ukighubikwa na vi-tendo vya rushwa. Sasa yule mwenye uwe-zo akichaguliwa anapitishwa na kamati kuu ndio maana napingana na mwenyekiti kid-ogo.

“Kinachotakiwa ili kuondokana na Gwaji-manisation katika chama, CCM ihakikishe wote wanaopita kwa misingi ya rushwa katika mchakato wa kura za maoni waengu-liwe katika mchujo ili kuwaweka wenye sifa. Maana akipitishwa asiyekuwa na sifa au mwenye uwezo, uzoefu unaonyesha anakuwa hana mpango wa kuwatumikia wananchi,” amesema Manyeko.

Mchambuzi mwingine wa siasa, Kiama Mwaimu amesema tatizo linaanzia katika mchakato wa kura za maoni ndiko kwenye shida kubwa, akidai wagombea wenye uwezo wa kifedha ndio wanaopenya na kuibuka washindi.

“Hawa wenye fedha utakuwa wanamiliki wajumbe karibu wenye katika mkutano wa kura za maoni, sasa ni ngumu wale wasi-okuwa na fedha kuibuka kidedea. Ndio maana mtu utasikia mgombea anayeongo-za ni fulani lakini hana sifa, lakini akifika vikao vya juu, jina lake halikatwi anarejeshwa kuwania.

“CCM inapaswa kuangalia upya mfumo wa kura za maoni ndio unaoleta shida hasa kwa wagombea wenye uwezo, lakini ha-wana fedha za kushawishi wajumbe ili kupenya,” amesema Mwaimu.



OSZAR »