Kariakoo Derby yasogezwa mbele, kupigwa Juni 25

Muktasari:
- Mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara 184 baina ya Yanga na Simba ulipangwa kuchezwa Juni 15 mwaka huu baada ya kuahirishwa Machi 8, 2025.
Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imesogeza mbele mechi ya Ligi Kuu namba 184 baina ya Yanga na Simba uliopangwa kuchezwa Juni 15 hadi Juni 25.
Taarifa hiyo imetolewa leo, Ijumaa, Juni 25 na TPLB.
“BODI ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imeusogeza mbele mchezo namba 184 wa
Ligi Kuu ya NBC kati ya klabu ya Yanga na klabu ya Simba ambao ulipangwa kufanyika kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa Juni 15, 2025 kuanzia saa 11:00 jioni.
“Mchezo huo sasa utafanyika Juni 25, 2025 kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa kuanzia saa 11:00 jioni.
“Bodi inazitakia mandalizi mema klabu za Yanga na Simba kuelekea mchezo huo,” imefafanua taarifa ya TPLB.
Taarifa hiyo ya TPLB imetolewa muda mfupi baada ya kusambaa kwa picha zinazomuonyesha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akiwa na viongozi wa Simba na Yanga, Ikulu Dodoma baada ya kufanya nao mazungumzo.