Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mfanyakazi wa Diddy atoa ushahidi, asimulia aliyoyaona ndani

Muktasari:

  • Kaplan alieleza kuwa alifanya kazi kwa rapa huyo kuanzia mwaka 2013 hadi 2015, kwa mshahara wa dola 125,000 kwa mwaka. Huku akifanya kazi hizo kwa saa 80 hadi 100 kwa wiki. Akiwa kazini hapo, anadai Diddy alikuwa akimtishia kumfukuza kazi kutokana na upole wake

Marekani. Wakati mashahidi wakiendelea kuongezeka mahakamani kufuatia kesi inayomkabili mwanamuziki Diddy. Hatimaye aliyekuwa mfanyakazi wake binafsi, George Kaplan, jana Mei 21,2025 alitoa ushahidi katika kesi hiyo huku akidai alitumika kuandaa vyumba kwa ajili ya matukio ya kingono.

Kaplan alieleza kuwa alifanya kazi kwa rapa huyo kuanzia mwaka 2013 hadi 2015, kwa mshahara wa dola 125,000 kwa mwaka. Huku akifanya kazi hizo kwa saa 80 hadi 100 kwa wiki. Akiwa kazini hapo, anadai Diddy alikuwa akimtishia kumfukuza kazi kutokana na upole wake.

Aidha alieleza alitumika katika maandalizi ya vyumba vya Hoteli za kifahari kama InterContinental iliyopo Los Angeles na Trump International huko New York kuhakikisha anaandika jina la ‘Frank Black’ ambalo hulitumia Diddy kuingia kwenye hotel.

Alisema alikuwa pia anaandaa mabegi yaliyojaa vitu vyote vya msingi kwa ajili ya ngono kama mishumaa, mafuta lainishi ya Astroglide, mafuta ya watoto ya Johnson & Johnson, na vinginevyo kisha kuyapanga ndani ya vyumba vya hoteli.

Vile vile alitumika kusafisha vyumba vya hoteli baada ya matukio hayo ya kingono kukamilika huku akidai alitumika kusafisha kwa lengo la kulinda jina la Diddy na siri zinazofanyika zisionekane na wafanya usafi wa hoteli hizo. Alikusanya chupa za mafuta ya watoto, pombe, na vinywaji vya Gatorade mara moja aliona poda ya kahawia iliyoganda juu ya sinki la bafuni.

Mbali na hayo Kaplan aliweka wazi wakati mwingine alitumwa kununua dawa mbalimbali, ikiwa ni pamoja na MDMA, ketamine na Advil  kwenda kuziweka katika hoteli.

Mpaka kufikia sasa zaidi ya mashahidi watano wameshatoa ushahidi kesi dhidi ya Diddy akiwemo aliyekuwa mpenzi wake Cassie Ventura, Mama wa Cassie Ventura, Dr. Dawn Hughes, Gerard Gannon. Huku msanii Kid Cudi akitarajiwa kutoa ushahidi kuhusu vitisho alivyopokea kutoka kwa Diddy baada ya kugundua uhusiano wake na Cassie.

Ikumbukwe Sean "Diddy" Combs alikamatwa Septemba 16, 2024 katika hoteli ya Park Hyatt, Manhattan, New York, baada ya kufunguliwa mashtaka ya shirikisho yanayohusisha njama ya kihalifu (RICO), usafirishaji wa binadamu kwa ajili ya ngono kwa nguvu, udanganyifu au kulazimisha na kusafirisha watu kwa ajili ya biashara ya ngono.

Kabla ya kukamatwa kwake nyumba za msanii huyo nyumba zake zilifanyiwa upekuzi na maafisa wa Idara ya Usalama wa Ndani (Homeland Security Investigations - HSI)  Machi 25, 2024. Upekuzi huo ulifanyika katika nyumba zake mbili ya Holmby Hills huko Los Angeles na ya Star Island huko Miami Beach.

Katika upekuzi huo vilipatikana vitu mbalimbali ikiwemo bunduki aina ya aina ya AR-15, midoli ya ngono, viatu virefu vya kisigino (stilettos), vifaa vya BDSM, na zaidi ya chupa 1000 za mafuta ya watoto na vilainishi, madawa ya kulevya na vinginevyo.

Mpaka kufikia sasa msanii huyo amekana mashitaka yote na endapo atakutwa na hatia atakabiliwa na kifungo cha maisha jela.


OSZAR »