Usiyoyajua kuhusu msanii Roma

Muktasari:
- Miaka zaidi ya 10 katika Bongofleva Roma ametengeneza ngoma kubwa zilizoacha alama, ameshinda tuzo, amefanya baadhi ya miradi inayoigusa jamii na hadi sasa ana albamu moja. Huyu ndiye Roma
Dar es Salaam. Ni miongoni mwa wasanii wachache wa Hip Hop Bongo ambao muziki umekuwa daraja la kufikisha ujumbe kutoka kwa umma kwenda kwa watawala, kwa kifupi Roma anaisemea jamii iliyomuamini na kumfanya kuwa chapa.
Miaka zaidi ya 10 katika Bongofleva Roma ametengeneza ngoma kubwa zilizoacha alama, ameshinda tuzo, amefanya baadhi ya miradi inayoigusa jamii na hadi sasa ana albamu moja. Huyu ndiye Roma.
1. Wimbo uliomtoa Roma kimuziki, Tanzania (2007) ulirekodiwa katika studio mbili taofauti, M Lab (Music Laboratory) na baadaye Tongwe Records ambapo toleo (version) la mwisho ndipo lilifanyika na kutoka na historia kuandikwa.

2. Unapaswa kujua kuwa wimbo wa kwanza kwa Roma na Stamina kufanya pamoja ni Mungu Yupo (2014) wakishirikiana na Walter Chilambo na Maunda Zorro. Kolabo hii ilikuja baada ya kukutana katika tamasha la Fiesta na wakati huo hawakuwa na mpango wa kuunda kundi.
3. Wimbo wa Roma, Mathematic (2012) ambao ndio ulimpatia umaarufu zaidi, kipindi unatoka ndipo alikuwa anahitimu Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) aliposomea Computer Science, taaluma ambayo Rapa Nikki Mbishi anayoa pia.
4. Matonya alipaswa kuwepo katika wimbo wa kundi la Roma na Stamina (Rostam), Now You Know (2018) ft. Khaligraph Jones, na alisharekodi wakiwa Nairobi, Kenya ila sauti yake ikaja kuondolewa dakika za mwisho kabla wimbo huo kutoka.
5. Video ya wimbo wa Roma, Diaspora (2020) ft. Lady Jaydee imefanyika katika nchi mbili tofauti, Tanzania na Marekani. Wakati video ya Shilole, Malele (2015) imefanyika katika nchi tatu ambazo ni Tanzania, Uholanzi na Ubelgiji.
6. Na kipande cha Lady Jaydee katika video hiyo ya Roma, kimeshutiwa eneo ambalo wasanii kibao wamefanya video zao hapo. Miongoni mwao ni Marioo, Ifunanya (2018), Navy Kenzo, Fella (2018), Alikiba, Ndombolo (2018) na Rosa Ree, One Way (2018).

7. Stamina alikuja kurudia kurekodi verse yake Bongo katika wimbo wa kundi la Rostam, Now You Know (2018) baada ya kuona kile alichofanya Khaligraph Jones katika ngoma hiyo ni moto, hivyo hakutaka unyonge hata kidogo.
8. Kabla ya Stamina kujiunga na Roma na kuanzisha kundi la Rostam, awali alikuwa katika kundi la Mtu Chee pamoja wenzake wawili, Country Boy na Young Dee aliyekuja kujitoa na nafasi yake kuchukuliwa na Young Killler.
9. Tuzo ya kwanza ya Roma kushinda katika muziki ni kutoka Tanzania Music Awards (TMA) 2013 aliposhinda kama Msanii Bora wa Hip Hop na Wimbo Bora wa Hip Hop (Mathematic).

10. Ilichukua miaka takribani 10 hadi msanii mwingine wa Hip Hop kushinda vingele vyote viwili kwa mpingo, naye ni Rosa Ree aliyeshinda TMA 2022 kama Msanii Bora wa Hip Hop na Wimbo Bora wa Hip Hop (Blue Print) akiwa ni msanii wa kwanza wa kike