Haya hapa majina ya vijana waliochaguliwa kujiunga JKT

Muktasari:
- JKT yatoa majina ya wanafunzi waliohitimu kidato cha sita watakaopaswa kujiunga na mafunzo ya kijeshi mwaka 2025.
Dar es Salaam. Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) limetoa orodha ya wanafunzi waliomaliza kidato cha sita mwaka 2025 watakaotakiwa kujiunga na mafunzo ya lazima ya kijeshi kwa mujibu wa sheria, huku vijana hao wakipangiwa kambi mbalimbali nchini.
Kwa mujibu wa orodha iliyotolewa na JKT, vijana kutoka shule mbalimbali za sekondari nchini wamepangiwa katika kambi tofauti ikiwemo Bulombora, Rwamkoma, Msange, Kanembwa, Makutopora, Mpwapwa, Ruvu, Nachingwea, Oljoro, Kibiti na Maramba.
Wanafunzi walioitwa wanatakiwa kuripoti katika kambi walizopangiwa kuanzia tarehe ambayo itatangazwa rasmi na mamlaka husika.
Aidha, JKT imeeleza kuwa hatua hiyo ni sehemu ya mpango wa kitaifa wa kuwajengea vijana uwezo wa kiakili, mwili na maadili ili waweze kuchangia maendeleo ya taifa.
Mafunzo haya yamekuwa yakitolewa kila mwaka kwa wanafunzi waliomaliza kidato cha sita kama sehemu ya kuwaandaa kiuzalendo na kuwapa stadi mbalimbali za maisha.