Mwanaharakati Atuhaire akutwa mpakani mwa Uganda, Tanzania

Mtetetezi wa haki za binadamu kutoka Uganda, mwanahabari na mwanaharakati, Agather Atuhaire.
Muktasari:
- Agather Atuhaire ni mmoja wa wanaharakati waliofika nchini kwenye kesi ya Mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu.
Dar es Salaam. Mtetetezi wa haki za binadamu na mwanaharakati kutoka Uganda, Agather Atuhaire, ambaye inadaiwa aliwekwa kizuini nchini Tanzania pamoja na Boniface Mwangi kutoka Kenya, amepatikana.
Agather amepatikana akiwa eneo la Mutukula ulipo mpaka wa Tanzania na Uganda usiku wa Alhamisi Mei 22, 2025, na tayari familia yake na mawakili wake wamethibitisha.
Hata hivyo, mamlaka za Tanzania mpaka sasa hazijaeleza chochote kuhusiana na matukio ya kuwekwa kizuizini kwa wanaharakati hao, huku zikikiri kuwazuia kuingia nchini mwanasiasa wa Kenya, Martha Karua na Jaji mkuu wa zamani wa nchi hiyo, Willy Mutunga. Viongozi hao walizuiwa kuingia nchini wakiwa Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere (JNIA) kabla ya kurudishwa nchini kwao.
Endelea kufufuatilia Mwananchi na mitandao yetu